Jumanne, 25 Machi 2014

UTALII:historia yake

 Mpenzi msomaji karibu kwenye blogu yangu  mpya ya taliikwetu .blogspot.com ambayo itakuwa ikielezea mambo mbalimbali kuhusu utalii wetu wa Tanzania.


Utalii ni kivutio kwa watu mbalimbali kwa lengo la kusoma, kujifurahisha, kujifunza ,kufanya uchunguzi  kutokana na mazingira anayotembelea mtu.


Katika blogu yangu nitagusia jinsi wanyama pori walio katika hifadhi zetu  wanavyouawa na majangili  kila kukicha ambao wanyama hao ni adimu mbugani huko.Wanyama hao ni tembo ,kifaru na twiga. Mbali na hayo nitaelezea mambo mengine ya utalii wetu jinsi unavyokua.


Nitazungumzia jinsi wanyama hao wanavyowindwa mbugani na wewe msomaji wangu utashauri nini kifanyike ili kuhakikisha wanyama pori wetu  hawauliwi ovyo kwa kutoa maoni yako.


Mpenzi msomaji wangu ninakukaribisha kwa moyo mkunjufu  katika blogu yangu kwa kutoa ushauri,maoni, kushare na kulike picha pamoja na habari iliyokuvutia.


Homely welcome

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni