Utalii,aghalabu, ni kuhusu kuona. Hivyo vya kuonja (utalii wa vyakula), kusikia (utalii wa kiutamaduni, hasa muziki) ni vitu vinavyokuja baadaye.
Moja ya changamoto zinazokabili sekta ya utalii ni utangazaji wa ndani na nje Sekta hii kwa kweli ni muhimu sana katika maendeleo ya nchi, lakini mfumo wa utangazaji iliwateja waweze kujua vivutio vilivyoko bado haujaendelea sana.
Lakini mtalii, kimsingi huja kutaka kushuhudia mambo ambayo amesikia habari zake, au ameona kupitia matangazo, hasa ya picha (za mnato na za kujongea- video).
Wakati hilo ni muhimu lakini matumizi ya video na picha kuvutia utalii kwa humu ndani yako kwa kiwango cha chini sana.
Ngorongoro, kwa mfano, wengi tunaisikia kwa jina, uhamaji wa wanyama kule Serengeti, tunasikia kwa jina tu, lakini hakuna mfumo mzuri wa kipicha wa kuwaonyesha wananchi. Sababu kubwa ni kuwa vyombo vya habari nchini haviweki maeneo ya utalii kama sehemu muhimu ya habari zao na hivyo tuwe tunaoneshwa mara kwa mara.
Aidha vyombo vya habari haviweki ratiba ya kutembelea au kuwepo kwenye maeneo ya tukio- wanyama wanapohama, ili kuwaonesha wananchi nini kinatokea na hivyo kuwajengea hamasa ya wananchi nao kuwa katika eneo la tukio katika msimu mwingine.
Lakini kikwazo kikubwa ni kuwa nchi kwa ujumla haijaweka mkazo mkubwa wa kutumia picha kama moja ya njia ya kuweka kumbukumbu za kitaifa. Na kwa sababu hiyo mafunzo katika picha nchini – mfano kwenye vyuo vya uandishi wa habari na vyuo vikuu, hayafikiriwi kabisa, isipokuwa ni kama kwa ajili ya uandishi wa habari za magazeti na televisheni.
Lakini somo la picha katika upana wake na ukuzaji utalii, hakuna mkazo kimafunzo. Juhudi zangu binafsi pale Chuo Kikuu panatakiwa kuwahamasisha wafanyakazi kuweka mafunzo ya picha bado zinagonga mwamba kwa sababu ya kutoona umuhimu wake licha ya kuwa mtaala unaainisha uwepo wa kozi hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni