Mwandishi wetu.
Shirika la Hifadhi za Taifa limeanza rasmi kutumia mfumo wa jeshi usu kutoka ule wa kiraia katika utendaji kazi wake ikiwa ni hatua mojawapo ya kuongeza ufanisi katika shughuli za uhifadhi.
Jumla ya wahifadhi 40 walihitimu mafunzo ya awamu ya kwanza ya kubadili mfumo wa utendaji kazi kutoka ule wa kiraia kwenda wa jeshi usu kwa viongozi maafisa wa ngazi ya kati “Transformation Leadership Course for Middle Cadre Wardens” yaliyofanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi hivi karibuni.
Mfumo wa utendaji kazi kwa kijeshi-usu utalisadia shirika kuimarisha nidhamu ili kuboresha utendaji kazi hasa katika nyakati hizi ambapo changamoto kuu ya ujangili unaotumia silaha za aina mbalimbali za moto hasa za kivita inazidi kushika kasi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni