Utalii:ELIMU NA HAMASA KWA WATANZANIA ITAINUA UTALII WA NDANI.
Tanzania ni moja kati ya nchi ndani ya jumuia ya afrika mashariki na
afrika kwa ujumla yenye kupokea watalii kutoka pande mbalimbali za
dunia.
Watalii hao hufika na kutazma vivutio mbalimbali vilivyopo katika nchi ya Tanzania.
Wageni wengi huja Tanzania kwa malengo ya kupumzika, kufurahi,kufanya utafiti na kujifunza.
Wageni wengi wameonekana kuvutiwa na uzuri wa nchi ya Tanzania kutokana
na vivutio vyake kama mbuga za wanyama,milima,maziwa ,mabonde na mambo
mengine kibao ambayo hayapatikani katika nchi nyingine duniani isipokuwa
Tanzania.
Wageni wengi huja kuwatazama wanyama waliopo ktk mbuga zetu na hivyo kufurahi sana wanapowaona katika macho yao.
Kwa upande wawatanzania wenyewe,muamko wa kutembelea hifadhi au vivutio
vyetu umekuwa ni mdogo sana,hali inayopelekea watanzania wachache sana
kufika ndani ya hifadhi.
Hali hiyo inasababishwa na muamko mdogo wa wa watanzania juu ya
kutembelea ktk hifadhi na wengi wanaamini kuwa wazungu peke yao ndio
wanapaswa kufanya utalii.
Hayo yanasababishwa na mambo mengi ikiwemo kukosekana kwa elimu juu ya utalii wa ndani na wakati mwingine hali ya uchumi nayo inachangia kwa
kiasi kikubwa kusababisha uwepo mdogo watalii wa ndani.
Kuna baadhi ya watanzania ambao wanauwezo wa kufika ndani ya hifadhi
lakini bado na wao hawafiki kutokana na kutopewa elimu na hamasa ya
kufika na kuzitembele hifadhi
.
Kuna muonekano mkubwa,kuwa wanafunzi kwa asilimia kubwa ndio wanaotembelea ndani ya mbuga za wanyama kuliko watu wazima.
Elimu ya utalii iwapo itatumika vizuri itachangia kukuza na kuinua utalii wa ndani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni