Alhamisi, 3 Aprili 2014

ASKARI 96 WA WANYMA PORI WAHITIMU ; WAAHIDI KUPAMBANA NA UJANGILI

Jumla ya  Askari 96 wa  Shirika  la Hifadhi la Taifa  la Wanyama Pori  (TANAPA) wametimu    mafunzo  ya miezi   mitatu  katika  chuo     kipya   cha wanyama   pori   cha Mlele  kilichopo   Mkoa  wa Katavi  na kutoa  kiapo cha utii  mbele ya Mkurugenzi mkuu  wa TANAPA Allan Kijazi
Askari hao  wa TANAPA walimaliza  mafunzo  hayo  hapo juzi  kwenye chuo  hicho   cha  wanyama Pori  cha Mlele  ikiwa ni  mafunzo ya  kwanza  hapa  nchini  kwa TANAPA  kutoa  mafunzo kama hayo kwa Askari wa wanyama pori kupatiwa mafunzo hayo  kabla ya kuanza  kazi
Katika  Risala yao ya  wahitimu wa mafunzo hayo  ya kulinda maliasili  iliyosomwa  na Bruno  Mbunda  walieleza kuwa wamejifundisha  mbinu mbalimbali za kulinda   rasilimali za Taifa  kwa Vitendo   na nadharia
Waliyataja baadhi ya mafunzo waliyoyapata kuwa ni namna ya kufanya doria , kukamata  wahalifu,  kumpekua  mhalifu  na kutotumia  nguvu  sana  katika kukamata  mhalifu      pia wamejifunza namna ya kutumia silaha.
Walieleza  katika kipindi hicho cha  mafunzo    wahitimu   hao walifanikiwa kukamata  wahalifu  50  wakati  wakifanya  doria  katika maeneo mbambali ya Mbuga ya  Katavi  na kwenye mapori ya akiba ya Rukwa  Lwafi
Wahitimu hao walieleza kuwa  mafunzo hayo yaliwashirikisha  Askari  99  lakini  watatu kati yao wameshindwa  kuhitimu  zikiwemo  sababu  mbambali  kama  utoro na utovu  wa nidhamu   hali ambayo ilfanya wahitimu  waliomaliza kubaki  96 ambapo kati yao mwanamke  ni mmoja  na wanaume ni  95
Kwa upande wake mkuu wamapori ya akiba  ya  Rukwa Lwafi  Joseph Mbung’ombe alimweleza mkurugenzi mkuu wa TANAPA kuwa chuo hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali.
 
Alizitaja changamoto hizo kuwa ni ukosefu wa mawasiliano  na  ubovu wa miundo  mbinu ya barabaa  na  upungufu  wa  magari pamoja  idadi ndogo ya washiriki  wa mafunzo kwa wanawake na ufinyu  wa bajeti
Nae  Mkurugenzi  wa Hifadhi  na Ikolojia  Martini  Loibook  alieleza kuwa mafunzo hayo walioyapata yanaumuhimu  sana  hasa kutokana na changamoto  zinazoikabili nchi  yetu  inayokabiliwa na wimbi la ujangili
Pia Mkurugenzi wa  utumishi   na utawalla   wa TANAPA  Witnes Shoo  aliwataka wahitimu hao  kufanya kazi  kwa uaminifu  kwa kujituma  na  wawe na nidhamu  na  wasiwe na tabia ya kutoa  siri za ofisi.
Mkurugenzi Mkuu   wa TANAPA  Allan Kijazi  aliwaasa wahitimu hao  wahakikishe wanafanya kazi  zao kwa uaminifu mkubwa  hasa  katika shughuli zao  katika kupambana kukomesha ujangili.
 
Aliwataka kutojihusisha  na masuala ya ujangili na badal awahakikishe wanafanya kazi za kupambana na mitandao ya ujangiri iliyopo ndani ya nchi na nje ya nchi
Alisema wapo baadhi ya watumishi wa TANAPA ambao wamekuwa sio waaminifu hivyo wahitimu hao wahakikishe wanafanya kazi zao kwa uaminifu pasipo kurubuniwa na mtu yoyote yule au watu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni