Wizara ya Maliasili na Utalii, imetaka kusitishwa kwa kodi mpya
ya vinyago ambayo imeanza kukusanywa hivi karibuni katika viwanja vya
ndege kwa watalii wanaoondoka nchini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,
Adelhelm Meru alitoa wito huo jana alipokuwa akizungumza na wauzaji wa
vinyago katika maduka ya Mount Meru Curios and Graft yaliyoteketea kwa
moto hivi karibuni.
Meru alisema wanataka kodi hiyo isitishwe kwani ni
kero kwa watalii na inaweza kuathiri biashara ya vinyago na ni kubwa
ikilinganishwa na bei ya kinyago.
“Kuna mtalii mmoja ametulalamikia kuwa amenunua
kinyago kwa Sh10,000, lakini anatakiwa kulipia kodi ya Sh30,000,
tumeamua kulifuatilia tatizo hili ili lifanyiwe marekebisho au kodi hiyo
iondolewe kabisa,”alisema Meru.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu,
alisema Wizara kupitia Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), itatoa pole
ya Sh100 milioni.
Mwenyekiti wa wafanyabiashara hao, Ally Kondo alisema moto huo umeteketeza maduka 223 ya wafanyabiashara ya vinyago.ambao vinyago vyao vyote vimeteketea na mali nyingine zikiwamo fedha katika maduka yao, Kondo aliishukuru Serikali na Tanapa kwa msaada walioutoa kwao toka walipopatwa na janga hilo.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni