Katika dunia ya utandawazi jamii hushindwa kuuza utamaduni wao, na chakula na upishi vikiwa moja ya tamaduni hizi.
Moja ya udhaifu mkubwa wa utangazaji wa utalii ni kukosa ushirikishwaji wa sekta mbalimbali za uchumi wa nchi.Kwa walio wengi utalii unafikiriwa katika ufinyu wake wa kiasili wa kwenda mbuga za wanyama na kutembelea magofu tuIli utalii ukamilike, kuna vipengele kadhaa
ambavyo lazima viende sawa kama vile vivutio vyenyewe, usafiri na huduma
za utalii, malazi na chakula.
.Ukiangalia blogu na tovuti nyingi Tanzania
utagundua kuwa zinatangaza vivutio vyenyewe tu, tena vile vyaasili, kwa
ukubwa zaidi, lakini chakula hakionekani kama kuwa ni sehemu muhimu
sana ya utalii.
Licha ya kuwa watalii wengi kiasili hutembelea
mahali kutaka kuona, karibu wote hupendelea kujaribish aladha mpya ya
vyakula na upishi wa asili katika maeneo wanayotembelea, na kwa hiyo ni
muhimu kuanza kufikiria uimarishaji wa utalii wa upishi
kwa kuwa tunaununua utamaduni huo, wanapata fedha
za kuanzisha mafunzo, matangazo na hatimaye tunafikiria kuwa kula
vyakula vya
huko ni bora zaidi.
Kumbe basi tukirahisisha na kuboresha
pishi na matangazo ya vyakula vyetu, tunaweza kutengeneza chanzo cha mapato kwa wananchi wetu
.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni