Tourism
Kwa habari mbalimbali za utalii .
Jumapili, 15 Novemba 2015
Jumatano, 11 Novemba 2015
Tanapa kuanza kutumia jeshi Usu
Mwandishi wetu.
Shirika la Hifadhi za Taifa limeanza rasmi kutumia mfumo wa jeshi usu kutoka ule wa kiraia katika utendaji kazi wake ikiwa ni hatua mojawapo ya kuongeza ufanisi katika shughuli za uhifadhi.
Jumla ya wahifadhi 40 walihitimu mafunzo ya awamu ya kwanza ya kubadili mfumo wa utendaji kazi kutoka ule wa kiraia kwenda wa jeshi usu kwa viongozi maafisa wa ngazi ya kati “Transformation Leadership Course for Middle Cadre Wardens” yaliyofanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi hivi karibuni.
Mfumo wa utendaji kazi kwa kijeshi-usu utalisadia shirika kuimarisha nidhamu ili kuboresha utendaji kazi hasa katika nyakati hizi ambapo changamoto kuu ya ujangili unaotumia silaha za aina mbalimbali za moto hasa za kivita inazidi kushika kasi.
Jumatatu, 7 Septemba 2015
Homely welcome to our tour company
2 Days 1 Night @ Tarangire National Park & Ngorongoro Crater for
Just us$ 630 Per Person for 2 Days & 1 Night at GIBBS FARM
1...Day 01: Pick from Hotel/Lodge or Airport, drive to Tarangire National Park with Lunch Box for Game Drive
Then drive to NGORONGORO GIBBS FARM for Dinner & Overnight
Day 02…Breakfast, drive to Ngorongoro Crater with Lunch Box for Crater Tour,
-Drive to Arusha for your flight
This price include Transport (Toyota Land Cruiser 4 X 4 Open roof), Breakfast, Lunch & Overnight,water, English/German/ Spanish Speaking guide and Park Fees
www.lovebirdsadventure.com / info@lovebirdsadventure.com
Mobile +255 768 520 557 (Luis Tarimo) or +255 752 524 073(Peter)
Skype: Luis Tarimo or Follow us on Twitter@Love Birds Advent
Dont hesitate to visit us through :
lovebirdsadventure.com
1...Day 01: Pick from Hotel/Lodge or Airport, drive to Tarangire National Park with Lunch Box for Game Drive
Then drive to NGORONGORO GIBBS FARM for Dinner & Overnight
Day 02…Breakfast, drive to Ngorongoro Crater with Lunch Box for Crater Tour,
-Drive to Arusha for your flight
This price include Transport (Toyota Land Cruiser 4 X 4 Open roof), Breakfast, Lunch & Overnight,water, English/German/ Spanish Speaking guide and Park Fees
www.lovebirdsadventure.com / info@lovebirdsadventure.com
Mobile +255 768 520 557 (Luis Tarimo) or +255 752 524 073(Peter)
Skype: Luis Tarimo or Follow us on Twitter@Love Birds Advent
Dont hesitate to visit us through :
lovebirdsadventure.com
Jumatano, 12 Agosti 2015
Serikali yamalizana na wapagazi
Moshi.
Mwandishi wetu.
Serikali imefikia maazimio saba yatakayowawezesha waongoza utalii na wapagazi kupata ujira wao stahiki na kwa wakati.
Katibu mteule wa Chama cha Waongoza Utalii (TGA), James Mong’ateko alisema hayo mjini Moshi jana.
Alisema miongoni mwa maazimio hayo ni wapagazi kulipwa asilimia 50 ya ujira wao kabla ya kuanza kufanya kazi.
“Hii ni sahihi kabisa wapagazi kabla ya kuanza safari zao ambazo huchukua kati ya siku saba hadi nane wataweza kuacha nyumbani fedha za matumizi,” alisema.
Alitaja maazimio mengine kuwa ni Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro kuzuia kampuni ambazo hazijasajiliwa kutoa huduma kwa watalii.
Alisema utekelezaji wa maazimio hayo utasaidia waongoza watalii na wapagazi kulipwa mishahara yao halali kwa mujibu wa Tangazo la Serikali, GN 228.
“Kulikuwa na kisingizio ya kuwa gharama kubwa za leseni wanazotozwa kampuni ya utalii ndiyo chanzo cha wao kuwalipa ujira ulio nje ya agizo la Serikali, lakini kwa azimio hili gharama hizo hazitakuwa sababu tena ya kunyimwa haki zetu za msingi,” alisema Mong’ateko.
Mwenyekiti wa TGA, Sadock Johnson aliiomba Serikali kupitia mamlaka zake husika kuhakikisha maazimio hayo yanatekelezwa kama ilivyoafikiwa na pande zote.
Wakili wa TGA, Elikunda Kipoko alisema wataunda kikosi kazi kitakachofuatilia kwa karibu utekelezaji wa maazimio hayo saba.
“Haina haja ya kumtafuta mchawi katika kukabiliana na changamoto zinazowakabili waongoza utalii na wapagazi tena, baada ya maazimio haya kupatikana kikubwa ni kuhakikisha utekelezaji wake unafanyika haraka kwa manufaa ya wahusika,” alisema Kipoko.
Jumatatu, 10 Agosti 2015
Jopo la majaji wakifanya ukaguzi wa michoro ya tembo
Jopo la majaji wa mashindano la kuchora na kuumba picha ya tembo yaliyoshirikisha wanafunzi wa shule za msingi jijini Arusha, wakihakiki kazi za wanafunzi hao.Picha kwa hisani ya Mtandao.
‘Vita dhidi ya ujangili ianzie shule za awali’
Arusha.
Mwandishi wetu.
Mratibu wa uhifadhi
kutoka Taasisi ya The Nature Conservancy inayojihusisha na masuala ya uhifadhi,
Alphonce Mallya alisema hiyo ni njia endelevu ya kukabiliana na ujangili
unaotishia kutoweka kwa tembo na faru.
Akizungumza katika
mashindano ya uchoraji wa picha ya tembo yenye ujumbe wa kupiga vita ujangili
kwa wanafunzi wa shule za msingi jijini Arusha jana, Mallya alisema jamii pia
inastahili kunufaika moja kwa moja na uhifadhi kupitia Serikali na taasisi
zinazohusika na miradi ya maendeleo ya rasilimali.
“Wananchi wanaoishi
maeneo ya karibu na hifadhi wataona ni jukumu lao kukabiliana na majangili
wanaotishia kutoweka kwa wanyama wetu iwapo watanufaika na miradi itokanayo na
mapato ya uhifadhi,” alisema Mallya.
Watoto Samuel
Godfrey, Ashraf Omar na Carlos Cosmas kutoka Shule ya Msingi Meru walioibuka
washindi katika mashindano hayo yaliyoshirikisha wanafunzi zaidi ya 600
waliwataka wenzao kuwa mabalozi wa vita dhidi ya ujangili kwa kuwafichua ndugu,
jamaa na majirani wanaoshiriki vitendo hivyo.
“Tukinyamaza
kuwataja majangili tutakuwa sehemu ya wahalifu huo na hatutaona wala kufaidi
urithi huu tuliojaliwa na Mungu,” alisema Carlos aliyekuwa mshindi wa jumla.
Watoto wengine
waliofanikiwa kufika fainali ni Mariamu Stephen, Frank Fredson na Mohammed Juma
wa Shule ya Msingi Burka, Doris Mollel, Godfrey Stephen na Ashraf Athmani
kutoka shule ya Ngarenaro.
Jaji Damarice
Kilaka alisema mashindano hayo yatafanyika kila mwaka ili kuwajengea uwezo
wanafunzi kuhusu hifadhi na vita dhidi ya ujangili nchini.
Jisajili kwenye:
Maoni (Atom)


