Arusha.
Mwandishi wetu.
Mratibu wa uhifadhi
kutoka Taasisi ya The Nature Conservancy inayojihusisha na masuala ya uhifadhi,
Alphonce Mallya alisema hiyo ni njia endelevu ya kukabiliana na ujangili
unaotishia kutoweka kwa tembo na faru.
Akizungumza katika
mashindano ya uchoraji wa picha ya tembo yenye ujumbe wa kupiga vita ujangili
kwa wanafunzi wa shule za msingi jijini Arusha jana, Mallya alisema jamii pia
inastahili kunufaika moja kwa moja na uhifadhi kupitia Serikali na taasisi
zinazohusika na miradi ya maendeleo ya rasilimali.
“Wananchi wanaoishi
maeneo ya karibu na hifadhi wataona ni jukumu lao kukabiliana na majangili
wanaotishia kutoweka kwa wanyama wetu iwapo watanufaika na miradi itokanayo na
mapato ya uhifadhi,” alisema Mallya.
Watoto Samuel
Godfrey, Ashraf Omar na Carlos Cosmas kutoka Shule ya Msingi Meru walioibuka
washindi katika mashindano hayo yaliyoshirikisha wanafunzi zaidi ya 600
waliwataka wenzao kuwa mabalozi wa vita dhidi ya ujangili kwa kuwafichua ndugu,
jamaa na majirani wanaoshiriki vitendo hivyo.
“Tukinyamaza
kuwataja majangili tutakuwa sehemu ya wahalifu huo na hatutaona wala kufaidi
urithi huu tuliojaliwa na Mungu,” alisema Carlos aliyekuwa mshindi wa jumla.
Watoto wengine
waliofanikiwa kufika fainali ni Mariamu Stephen, Frank Fredson na Mohammed Juma
wa Shule ya Msingi Burka, Doris Mollel, Godfrey Stephen na Ashraf Athmani
kutoka shule ya Ngarenaro.
Jaji Damarice
Kilaka alisema mashindano hayo yatafanyika kila mwaka ili kuwajengea uwezo
wanafunzi kuhusu hifadhi na vita dhidi ya ujangili nchini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni