Mabadiliko makubwa
Maliasili na Utalii


Lazaro
Nyalandu
Habari
zilizopatikana na kuthibitishwa na baadhi ya wakurugenzi waliohusika katika
uteuzi huo, zinaeleza kuwa mabadiliko hayo yalifanyika hivi karibuni na barua
za kutekeleza majukumu yao mapya walipewa juzi
Habari
zilizopatikana na kuthibitishwa na baadhi ya wakurugenzi waliohusika katika
uteuzi huo, zinaeleza kuwa mabadiliko hayo yalifanyika hivi karibuni na barua
za kutekeleza majukumu yao mapya walipewa juzi.
Hata
hivyo, Waziri wa wizara hiyo, Lazaro Nyalandu alipoulizwa kuhusu suala hilo
alisema atalizungumzia Jumatatu ijayo.
Taarifa
kutoka ndani ya wizara hiyo, zilieleza kwamba barua ya mabadiliko hayo
imeandikwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais -Utumishi, George Yambesi.
Akizungumza
na gazeti hili jana Yambesi alisema, “Taratibu za uteuzi wa wakurugenzi ndani ya
wizara ziko wazi kwamba zinafanywa na katibu mkuu wa wizara hivyo (Maimuna
Tarishi) hivyo naomba mtafuteni yeye.” Hata hivyo Tarishi hakuweza kupatikana
kuzungumzia mabadiliko hayo.
Katika
mabadiliko hayo, aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Wanyamapori, Profesa Alexander
Songorwa amepelekwa kuwa Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Afrika,
Mweka na mkurugenzi mpya ameteuliwa kuwa Herman Keraryo aliyekuwa mkurugenzi
msaidizi wa idara hiyo.
Aliyewahi
kuwa Mkurugenzi wa Matumizi Endelevu ya Wanyamapori, Profesa Jafari Kidegesho
amepelekwa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (Sua).
Dk
Charles Mulokozi aliyekuwa Kaimu Mkuu Msaidizi Matumizi Endelevu Wanyamapori
anabaki katika nafasi hiyo na Julius Kidede amepelekwa Ngorongoro kupangiwa
majukumu mengine ya kazi.
Mkuu wa
Kitengo Kidogo cha Migogoro cha Wanyamapori ameteuliwa David Kanyata na
Faustine Masalu akiteuliwa kuwa Mkurugenzi Uzuiaji Ujangili nchini, awali
alikuwa Mkuu wa Kikosi cha Kuzuia Ujangili Kanda ya Mashariki- Dar es Salaam.
Kwa
upande wake Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii, Mchungaji Peter Msigwa
akizungumzia mabadiliko hayo, alisema kubadilishwa kwa wakurugenzi hao ni jambo
zuri lakini haliwezi kuleta ufanisi endapo Ikulu itaendelea kuingilia utendaji
wa wizara hiyo.
“Bado
watendaji wa juu wanaingilia utendaji kazi wa wizara, katika hotuba yangu
bungeni nilipendekeza wakurugenzi hao kuchukuliwa hatua jambo ni jema, lakini
bado wizara hii ina matatizo lukuki ambayo ili kuyamaliza kunahitajika
kufanyika kwa ushirikiano wa wadau wote,” alisema Msigwa ambaye ni Mbunge wa
Iringa Mjini kupitia Chadema.
Akizungumzia
uteuzi huo, Keraryo alisema ameupokea kwa furaha na kuahidi kufanya kazi kwa
kuzingatia sheria na kanuni zinavyomtaka kutenda.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni